By Raphael Nyoni.
Msanii wa muda mrefu na ambaye ameweka maskani yake kule Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.Vitalis Maembe ametoa waraka. Waraka huo unaelezea mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na baadhi ya vitu vya kufanya ili kuiboresha Tanzania. Soma waraka Huo kama alivyoutuma kwa vyombo vya habari hapo chini.
Ndugu,
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Waziri mkuu, Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mawaziri wote wa kawaida, Mawaziri Vivuli na viongozi wote wa kiimani na kisiasa.
Heshima yenu popote mlipo!
Mswahili nawasalimia!
Mimi ni Vitali Maembe, mwanamuziki, Mswahili, Mwalimu na mtumishi mwenzenu wa waafrika.
Mnamo tarehe 03/02/2011 nilianza ya kugawa chanjo ya Rushwa, ubinafsi na uvivu kwa kutumia muziki kwa watu wote. Bila kutumwa wala kushinikizwa na mtu wala shirika, wala chama, nilianzia Bagamoyo, mitaani, viwanjani na katika shule njiani kuelekea Dodoma. Ilinichukua siku na wiki kadhaa kufika huko, namna ya kusafiri kutoka kituo mpaka kituo, ruhusa ya kufanya maonesho, vitisho, njaa vilikuwa vikwazo vikubwa.
Hatimaye jumatano tarehe 16 februari 2011 saa nne kasoro dakika kumi natatu mimi na rafiki zangu wawili tulifika Dodoma kituo kikuu cha mabasi. Lengo likiwa ni lilelile kuiokoa nchi yetu kwa jasho letu, akili yetu yote, moyo wetu wote na uwezo wetu wote kwa kadri tulivyoaminiwa na waswahili wenzetu, kwa kufikisha Waraka wa Chanjo wenye kurasa tano wenye ushauri na unaowaomba mawaziri na wawakilishi wafikirie namna ya kufanya marekebisho kadhaa yatakayoboresha huduma muhimu katika jamii. Ukosefu na uhaba wa huduma na haki unapelekea watanzania wengi kushiriki na kushirikishwa katika Rushwa. Hali ambayo inafanya waswahili tunatukanwa, tunatukana, kutukanishwa na kujitukanishwa, thamani ya utu wetu kutoonekana ndani ya nafsi zetu na nje katika kuishi kwetu, kwa kifupi sisi waathirika wa rushwa tunajiona kama mifugo tu kwenu nyinyi na wakati wowote mkiamua lolote mnatufanyia, tena mmeshafanya mengi kwa manufaa yenu na mifumo yenu bila kujali uwepo wetu”
Pia lengo lilikuwa ni kuwasilisha ujumbe kwa njia ya muziki, ujumbe ambao niliagizwa na watanzania wa kawaida.
Pamoja na kufika Dodoma hiyo jumatano ya tarehe 16 februari, hatukwenda moja kwa moja bungeni, tulipumzisha akili zetu, tukasema na njaa zetu, baada ya muafaka tarehe 17 asubuhi tulienda bungeni kuomba ruhusa kumuona Spika wa bunge ili kukabidhi waraka na kopi za albamu ya muziki ya Chanjo. Siku hiyo hatukufanikiwa kupata ruhusa, baada ya usumbufu mkubwa na vitisho getini kutoka kwa askari na wahusika wengine wa mlangoni jioni iliingia na siku ikaisha bila ruhusa. ‘haya ninayoyoyasema naamini mnayajua au mna taarifa nayo’ Hatukukubali kuondoka mpaka tulipopata ruhusa ya kukutana na msaidizi wa Spika Bw. Berege, hatukuweza kumkabidhi barua zetu sitini na nne zinazotakiwa kuwafikia mawaziri wote, wawakilishi wa vyama bungeni, spika na katibu wa bunge kwa kuwa msimamo wetu ulikuwa ni kumfikishia Spika na kumkabidhi ili kuhakikisha ujumbe unawafikia wahusika. Siku iliyofuata yaani tarehe 18 februari 2011, tulifika mapema asubuhi, mara hii tulipata ruhusa ya kuingia katika ofisi ya spika, haikuwa rahisi kuonana naye lakini tuliridhika na ukweli, hivyo tulikutana na Katibu wa spika Bw. Eliufoo na kumkabidhi ujumbe wetu aliupkea saa nne na dakika kumi na sita na akaandika na kuweka sahihi kwenye katatasi yetu nyeupe ya A4 aliyoamua kuikunja katikati kwa mapana baada ya kuandika kwa kalamu yake ya wino wa buluu kuwa amepokea ujumbe wetu.
Awamu ya kwanza ya Chanjo iliishia BASATA Baraza la Sanaa la Taifa. Watu wasiopungua Elfu Ishirini wamekwishapata Chanjo ya Rushwa, Ubinafsi na Uvivu.
Pamoja na hayo yote mpaka sasa sijapata matokeo ya ujumbe wangu Dodoma kutoka kwenu walengwa wote yaani wawakilishi wa vyama na Mawaziri wote. Spika na katibu wa bunge pia mmekaa kimya.
Sasa nawauliza hiyo ni dharau, kiburi au chuki? Na kama ni hasira au chuki mmeniwekea mimi au wananchi wenu?
Sikilizeni niwaambie,
Mnaweza kujiuliza kwanini nitumie gharama nyingi ya muda, pumzi na pesa yangu masikini kama mie na kung’ang’ania kuimba nyimbo za namna hii na kuwafikishia watu moja kwa moja, kueleka bungeni. Kwanini natumia pesa ambayo ingebidi niitumie kuwatunza wanangu wadogo nyumbani wanaosubiri msaada wangu, mimi ni mjinga? Mimi siijui raha ama sina haja ya kustarehe? kwanini nisifanye biashara ya muziki nikawa tajiri kama hao wanamuziki wengine mnao wafagilia? Kwanini nisiwapigie kampeni niwe mmoja kati yao wanaoahidiwa viwanja ili wawadanganye masikini waswahili hali wakijua ukweli ni upi?
Sina kingine zaidi ya mapenzi kwa nchi yangu na Afrika yangu, tumia akili na umri wako sasa kuelewa mambo mengine.
Lazima ufahamu kuwa Rushwa ndio asili ya mateso wanayoyapata watu wenu, amua leo, sema neno moja tu na watu watapona. Kwa taarifa yako mkuu, watu wanakuficha mimi nakuambia ukweli, Waswahili wanasema huwezi kuwafanya lolote wala rushwa na wezi wa nchi hii kwa kuwa wewe ni mwenzao mimi siamini hayo lakini waswahili wana misemo yao kama vile ‘Lisemwalo lipo…’ au ‘ngoma ikivuma sana…’ nk.. Wewe waswahili unawajua naomba uyatilie thamani maneno yao.
Wakuu!
Nilipoona kuwa kazi yenu ya kuongoza ni ngumu nikaona niwasaidie kurahisisha mambo fulani, lakini mnaniona mpumbavu kabisa, angalieni matusi mnayotukanwa, watu wanailaani siku waliyoenda kupiga kura kuwachagua. Mimi na waswahili wenzangu tumegundua kuwa nyinyi ugumu wa maisha haya ndio raha yenu, mateso ya watu hawa wanyonge ndio matumaini yenu ya maisha bora kwenu, na watoto wenu siku za mbeleni..
Nasema haya maneno yanayoshabihiana na lawama kwenu kwa kuwa naiona juhudi yenu ya kuwafanya watanzania wasisikie muziki wetu, muziki wa mswahili, muziki unaoeleza maisha halisi kabisa ya muafrika na kutoa ufumbuzi.
Tazama! Unawaunga mkono watu ambao wanaonekana wazi hata kwa macho ya kitoto kuwa hawana mapenzi ya kweli nasi, unatuuza watu wako kwa ushawishi wa vitu vidoogo kabisa katika maisha, Makaratasi, makaratasi tu ndiyo yanayokufanya utuone bidhaa, unampa shetani damu ya wanao! Unaiunga mkono kauli ya yule punguani mmoja wa Afrika ya kusini miaka 1980! Umesahau kabisa KIAPO chako kwa Mungu mbele ya Muumba na waswahili wote, umewasahau wazee wetu walivyoteseka na kudhalilika katika kuijenga Afrika hii?
Nakukumbusha!
Yule punguani wa Afrika ya kusini alivyosema,
“The black is the raw material for white man. So Brothers and Sisters, let us join hands together to fight against this Black devil. By now every one of us has seen it practically that the Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other. They are good in nothing else but making noise, dancing, marrying many wives and indulding sex. Let us all accept that the Black man is the symbol of poverty, mental inferiority, laziness and emotional incompetence”
Je, kwa haya mnayotufanyia leo hali mkiwa wasomi na mnajua yote haya mnafikiri uongozi wenu haukubaliani na huyu bwana? Je, mnawezaje kumshawishi mswahili akawaelewa kuwa hamtumii msimamo huu kuwaongoza waswahili?
Mswahili haitaji majibu ya ahadi bali vitendo na kauli thabiti itakayompa uhuru wa kweli katika ardhi ya babaake.
Tumewapa nguvu ya kutosha itumieni kutuokoa!
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri mkuu, Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano Tanzania, Mawaziri wote halisi na vivuli.
Najisikia vibaya kukupa ushauri huu lakini inabidi nikupe ingawa ni aibu kwangu na watanzania wote tuliokuweka madarakani, haya mambo ilibidi uwe umeyapitia na kuyafahamu miaka mingi iliyoita na kuyatumia kama ufahamu kukurahisishia nakuiboresha kazi yako ya kuwaongoza watu ambao wameletwa kuishi Afrika ili wasipate taabu, wafurahie maisha katika nchi waliyopewa na Mungu wao.
Sikiliza Mzee wangu!
Uliamua kuiongoza afrika na ukapewa ridhaa na waafrika, usikurupuke tu ukaanza kuongoza bila kujua wapi afrika inatokea, achana na hayo mavideo za ulaya na misimamo ya kigeni, acha kujiamini na elimujoho TANZANIA NI MOJA NA HAKUTAKUJA KUWA NA TANZANIA NYINGI ZAIDI YA HII YA WASWAHILI. Tanzania ndio Afrika, Afrika ndio dunia. Kama utafanya watanzania wakuone bora basi wewe utakuwa bora kuliko viongozi wote Duniani kwakuwa watanzania ni waswahili na waswahili wanafikiria mara tatu ya mtu wa kawaida.
Tuliza akili mkubwa unisikilize.
kwa kukusaidia tu ni kwamba ujue kuwa huna uwezo wa kuiongoza hata sehemu ndogo ya waafrika pekeyako, tena bila kujua haya nikwambiayo leo ndiyo kabisaa.
Niwie radhi mkubwa wangu kama utaona nakukosea kukwambia haya. Sikwambii haya kukushusha cheo chako, la, haya ni mapenzi tu. Nakuomba uupe heshima umri wangu, na kazi yangu kama mwanamuziki, mwalimu na mswahili kwa kusikia mafundisho yangu.
Kuna kitu kinaitwa Pan-africanism.
Ndani ya hiyo tafuta kujua kuhusu wanasiasa wake, viongozi, wanamuziki na watu wengine waliohusika na afrika kwa moyo wao wote. Mwanao nakuomba uyashike haya, kama huwezi kuhifadhi kichwani shika kalamu na uandike haya. Wengi wa hawa walifanya mambo mazuri lakini mimi nawewe hatujui nia za moyoni mwao, pia wapo wliofanya mabaya, kwa kuangalia walikoanzia mpaka wanakoishia utajua lipi linalokufaa.
Nenda ukamsome.
Nnamdi Azikiwe, Robert Mugabe, Amílcar Cabral, Muammar al-Gaddafi · Marcus Garvey, David Comissiong, Kenneth Kaunda, Samora Machel, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba, Thabo Mbeki, Abdias do Nascimento, Gamal Abdel Nasser, Oliver Tambo, Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, John Nyathi Pokela, Haile Selassie, Robert Mangaliso Sobukwe, Ahmed Sékou Touré, Abdulrahman Mohamed Babu, I.T.A. Wallace-Johnson
Usiache kumsoma.
Molefi Kete Asante, Steve Biko, Edward Wilmot Blyden, John Henrik Clarke, Cheikh Anta Diop, W. E. B. Du Bois, Frantz Fanon, John G. Jackson, Yosef Ben-Jochannan, Maulana Karenga, Fela Kuti, Bob Marley, Malcolm X, Ibrahim Hussein, Zephania Mothopeng, George Padmore, Motsoko Pheko, Runoko Rashidi, Walter Rodney, Burning Spear, David G. Mailu, Henry Sylvester-Williams, Stokely Carmichael, Omali Yeshitela
Tuliza akili yako ujue wamefanya nini na wamefanyiwa nini kwaajili ya afrika yao na kwaajili yao binafsi.
Usije ukawaongoza waafrika bila ufahamu mkubwa kuhusu haya yafuatayo, hapa ndipo kuna malengo, nia, utu na heshima yetu. Kuchanganyana na kuchanganyikana.
United States of Africa, Afrocentrism, Kwanzaa, Pan-African colours, Pan-African flag, Négritude ,African nationalism, African socialism, African Century · Africanization, Kawaida, Ujamaa, Harambee, Ubuntu, Zikism, Black nationalism.
Jua na uelewe kuhusu muungano, mabadiliko, umoja wetu na kudumu kwetu kama waafrika.
African Union, Organization of African Unity, Uhuru Movement, UNIA-ACL · African Unification Front, International African Service Bureau.
Hayo mambo mengine ni urembo tu, ni njia ya kutafuna rasilimali za waafrika tu. Nakuamini sana na ninaamini kuwa maneno yangu yatawasaidia watanzania na waafrika wenzangu kupitia busara zako, hayatakuwa chanzo cha wewe kunitesa au kugeuka sababu kuniua masikini mie ninayejaribu kuwakoa watanzania na waafrika wenzangu. Najua nimekupa nguvu ya kufanya lolote utakalo lakini naomba usinidhuru kwani wanangu na wapenzi wangu bado wananihidaji.
Mimi ni wanamuziki nisingependa haya yafikie huku lakini imebidi nitumie njia hii maana nimeimba sana lakini redioni hawapigi, wengi wao wanasema wanahofia utawala wenu, hautafurahia nyimbo za mafunzo, lakini labda ni uoga wao tu, nakuomba uwaruhusu basi wapige nyimbo za Vitali Maembe.
Mkuu,
Katika kuongoza yashike hayo yote lakini langu mimi ni moja tu kama si mawili, usiupe nafasi ubinafsi, ubaguzi wa rangi, dini, kabila na jinsia.
Mwisho,
Usiache muziki ukadhalilishwa, usiupromoti muziki ambao unaona wazi unawapeleka watu wako pabaya, nchi italaaniwa, Muziki mzuri ni ule unaotoa elimu njema na kuwasaidia watu, ule mwingine usiuue pia uache uwepo tu ili kutofautisha kizuri na kuzuri sana. ‘pasipo ndicho kilichopo ndicho?’
Mswahili anakutakia uongozi mwema na mafanikio katika mema!
‘Mungu ulisha ibariki Tanzania, Mungu ulisha ibariki Afrika! Tunaomba usituondolee Baraka hii!’
Thursday, April 21, 2011
Thursday, April 14, 2011
Power station ya mradi wa kijiji cha chamani
![]() |
Mzee Pwagu akielekea ilipo power station ya kijiji cha chamani, kijiji hicho kipo kilometa 15 kutoka ilipo power station ya mji mwema |
![]() |
Akifungua Mlango wa power station, pembeni ni kijana ambaye amepewa mafunzo na mzee Pwagu namna ya kutengeneza umeme na kukisimamia kituo hicho cha umeme. |
![]() |
Mashine ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji kama inavyoonekana. |
![]() |
Mashine hii inazalisha umeme wenye uwezo wa kutumika na kaya 50 katika kijiji cha chamani, lakini ni baadhi ya wanakijiji tu ndio ambao wamefikiwa na huduma hiyo |
![]() |
Mzee Pwagu akitoka toka power station huku akitaniana na vijana wake. |
Kuelekea Mji mwema ilipo Power station ilipo...
![]() |
Safari kuelekea ilipo power station |
![]() |
Power station inavyoonekana kwa nje |
![]() |
Akipima kiwango cha umeme unaozalishwa |
![]() |
Mtambo wa zamani kabla hajapata mafunzo toka kwa Injinia wa kijerumani jinsi ya kutengeneza umeme bila uharibifu wa mazingira |
![]() |
Power station |
![]() |
Maji yanayotoka nje baada ya kupita kwenye mota ya kuzalisha umeme. Maji haya huvunwa kutoka mtoni na kurudi tena mtoni baada ya kuzalisha umeme |
Wednesday, April 13, 2011
Mzee Pwagu:Injinia wa umeme Njombe asiyefahamika
Kuna watu wengi wanaoweza kuisaidia serikali kutatua tatizo la umeme kama watatumika ipasavyo.
Bahati mbaya serikali yetu inashindwa kuwatupia macho na kuwaacha waende na vipaji vyao,
huku taifa likizama katika giza. Mmoja wa watu wenye uwezo wa kuzalisha umeme John Mwafute,mwenye umri wa miaka 81anayefahamika zaidi kwa jina la Mzee Pwagu kutoka mjini Njombe.
Mzee Pwaguaada ya kumaliza elimu yake ya msingi alijifunza kazi ya uhunzi, kidogo kidogo akaanza kujifunza na mambo ya umeme. Alipopata ujuzi katika uhunzi na umeme, akaanza kubuni vifaa mbali mbali ambavyo vilikuwa vinamsaidia katika kazi zake za uzalishaji umeme wa maji.
Alianza kwa kuzalisha umeme wa kilowatt 1.
Baada ya kuona juhudi zake na uwezo wake wa kuzalisha umeme, akapata mafunzo zaidi kutoka kwa Godfrey Ndeo kwenye mambo ya uinjinia.
Hivi sasa anazalisha umeme wa" phase 3" ambao una uwezo wa kuendesha kiwanda, lakini anautumia katika karakana yake iliyopo Mji mwema, nje kidogo ya mji wa njombe.
Mzee Pwagu, ameamua kuwafundisha vijana juu ya ujuzi alionao. Kwa kuanza ameanza navijana walio kijiji cha Chamani, kilometa Kumi na tano kutoka njombe mjini.
Lengo lake ni kuwafikishia umeme watu wa vijijini na sehemu zote ambazo serikali imezisahau, katika huduma ya umeme.
Mafunzo kwa vijana wa kijiji cha chamani yamechukua muda wa mwaka mmoja hadi kukamilika na hivi sasa nao wanafurahia umeme uliozalishwa nao kwa msaada wa mzee Pwagu
Mzee Pwagu ni changamoto kubwa kwa "Dowans" na serikali kuhusiana na suala zima la tatizo la umeme.

![]() | ||||||||||
Mzee Pwagu |
![]() |
"Ngoja nikuonyeshe kijana" |
![]() |
"Umeona mambo yangu ?Hili trela tu picha linakuja"Mzee Pwagu akimuuliza Raphael Nyoni, mwanahabari toka chuo kikuu cha Tumaini,Iringa |
![]() | ||
Hapa anasema "haya sasa twende nikupeleke kwenye power station" |
Monday, April 11, 2011
Maazimisho ya 17 ya mauaji ya Kimbari 1994 Rwanda yaliyofanyika katika chuo kikuu cha Tumaini Iringa
- Mgeni rasmi Mhe. Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda
- Mdegela awaasa wanasiasa wa Tanzania kuacha ubinafsi
Mkuu wa kitivo cha sheria Renatus Mgongo, Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Lazaro Nyalandu na Askofu wa KKKT-Iringa Dr. Owdenburg Mdegela alipowasiri chuo kikuu cha Tumaini-Iringa |
Katika ukumbi wa Multipurpose |
Askofu Mdegela akimnong'oneza waziri Nyalandu |
Wakitoa heshima ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari |
Mkuu wa kitivo cha sheria akiwakaribisha na wageni katika hafra |
Mkuu wa chuo Prof. Nicolas Bangu akifungua hafra ya maadhimisho ya mauaji ya Kimbari |
Mhadhili wa sheria akiwasilisha mada kuhusu sheria ya Kimataifa |
Mwanasaikolojia na mhadhili wa saikolojia katika chuo kikuu cha Tumaini Mch. Mutha Ruiza akiwasilisha mada juu ya athali za kisaikolojia zilizotokana na mauaji ya Kimbari |
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini |
Usikivu! |
Umakini |
Ni wakati wa wasikilizaji nao kuchangia hoja, Huyu ni Mhadhili wa sheria akichangia hoja juu ya sheria ya kimataifa |
Mhadhili wa chuo kikuu cha Tumaini akichangia hoja juu ya matatizo ya kisheria yayolikumba bara la Afrika |
Godwin Kunambi akichangia hoja |
Kanyolo pia alikuwepo |
Wakiagana mwisha wa hafra |
Wednesday, March 16, 2011
Tuesday, March 15, 2011
Tuesday, March 1, 2011
HOTUBA YA MHE. RAIS KWA WANANCHI – 28.02.2011
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,
KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011
Ndugu Wananchi,
Kama ilivyo ada naomba kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma kwa kutujaalia fursa nyingine ya kuzungumza kwa kutumia utaratibu tuliojiwekea wa kila mwisho wa mwezi. Leo nina mambo matano ambayo ningependa kuyazungumzia.
Milipuko ya Mabomu Gongolamboto
Ndugu Wananchi;
Jambo la kwanza ni lile tukio la usiku wa tarehe 17 Februari, 2011 la milipuko ya mabomu iliyotokea katika ghala kuu la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania lililoko Gongolamboto, Dar es Salaam. Pamoja na kuharibu majengo mengi yanayohifadhi zana na vifaa muhimu vya Jeshi letu, milipuko hiyo imesababisha vifo vya Watanzania wenzetu 25 na wengine 512 kujeruhiwa. Aidha, mali na nyumba kadhaa za raia zimeharibiwa kwa viwango mbalimbali.
Siku iliyofuata Baraza la Usalama la Taifa lilikutana kujadili tukio hilo na kuagiza hatua mbalimbali za kuchukuliwa kushughulikia athari za maafa hayo. Mara baada ya kikao hicho nililitangazia taifa maamuzi tuliyofanya. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi maalum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu hususan Kitengo cha Maafa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Madaktari na Wauguzi wa Hospitali za Amana, Temeke na Muhimbili na nyinginezo pamoja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri ya kutekeleza maagizo ya Baraza la Usalama la Taifa.
Maiti wote 25 wameshazikwa kwa gharama ya Serikali kule ambako ndugu waliamua wakazikwe. Kwa ajili hiyo maiti 10 wamezikwa Dar es Salaam na wengineo mikoani kama ifuatavyo:-, Mara – wanne, Pwani – watatu, Tanga - wawili, , Lindi – mmoja, Kagera - mmoja, Kilimanjaro – mmoja, Mbeya – mmoja na Mtwara – mmoja. Majeruhi wameendelea kupatiwa matibabu na huduma stahili. Mpaka sasa kuna majeruhi 36 ambao bado wamelazwa katika hospitali za Amana, Temeke na Muhimbili. Watoto 857 waliopotezana na wazazi wao wameshaunganishwa na familia zao. Hata hivyo, watoto 15 bado hawajatambuliwa na wazazi au walezi wao. Kwa sasa watoto hao wamepelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto cha Kurasini. Napenda kuwakumbusha wazazi waliopotelewa na watoto kufika kituoni hapo kuwatambua watoto wao. Ni jambo la kustaajabisha kwamba zaidi ya siku kumi sasa zimepita wazazi au walezi hawajajitokeza kutafuta watoto wao.
Ndugu Wananchi,
Ndugu zetu 539 katika kaya 115 hawana makazi kutokana na nyumba zao kuharibiwa na mabomu. Wamepewa hifadhi ya mahema yaliyojengwa pembeni mwa makazi yao. Aidha, wamepatiwa mavazi, magodoro, mashuka na mablanketi. Kadhalika wanapatiwa huduma za chakula, maji na mengineyo. Pamoja na mchango wa Serikali, wapo watu na mashirika mbalimbali yaliyotoa michango mbalimbali kusaidia waathirika hao. Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani nyingi sana kwa moyo wao wa upendo, ukarimu na huruma kwa ndugu zetu hao ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu yasiyotarajiwa. Inshaalah Mola atawalipa maradufu kila mlichopunguza. Narudia tena uamuzi na ahadi ya Serikali ya kuendelea kuwahudumia mpaka hapo watakapofidiwa kwa uharibifu wa nyumba zao na mali zao.
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa agizo la kutambua na kufanya tathmini ya nyumba zilizoharibiwa unaendelea kufanywa kwa nia ya kuwafidia ipasavyo. Kwa upande wa fidia tumeamua kuwa Serikali ibebe jukumu la kujenga upya nyumba hizo kwa mujibu wa kiwango cha uharibifu. Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia Shirika lake la Uchumi. Nimeamua hivyo ili kuhakikisha kuwa maisha ya ndugu zetu waliokumbwa na maafa haya yanarejea kuwa ya kawaida mapema iwezekanavyo. Aidha, nimeagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ishirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Taifa cha Maafa kuhakikisha kuwa utekelezaji unaanza mapema iwezekanavyo.
Ndugu Wananchi,
Jeshi la Ulinzi la Wananchi lilipewa kazi kubwa tatu. Kwanza, madaktari na wauguzi wa Jeshi washiriki katika kusaidia kutoa huduma kwa wananchi waliojeruhiwa. Nafurahi na kupongeza kwamba jambo hili limetekelezwa vizuri. Pili, kuokota na kukusanya mabomu ambayo hayakulipuka na vipande vipande vya mabomu yaliyolipuka kutoka maeneo wanayoishi raia. Kazi hiyo nayo imefanyika na inaendelea kufanyika. Mpaka tarehe 25 Februari, 2011, Wanajeshi wamekusanya zaidi ya mabomu na vipande 3,013. Yapo maombi ya wananchi kuwa kasi ya ukusanyaji iongezwe, ujumbe huo umeshafikishwa kwa viongozi wa Jeshi.
Ndugu Wananchi;
Jukumu la tatu ambalo ni wajibu wao kufanya, ni kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina unafanywa kuhusu chanzo cha milipuko hiyo. Nimearifiwa na Mkuu wa Majeshi kuwa Bodi ya Uchunguzi imekwishaundwa. Wakati huo huo lile agizo la Baraza la Usalama kuwa wataalamu wa nchi za nje nao washirikiswe katika uchunguzi limetekelezwa. Serikali ya Marekani imetoa wataalamu kutoka Jeshi lake kusaidia katika uchunguzi. Ni imani yangu kuwa uchunguzi wa makundi haya mawili kila moja kwa wakati wake huenda utasaidia kupata ukweli. Napenda kutumia nafasi hii kuwasihi Watanzania wenzangu kuwa na subira na kuacha tabia za kueneza uvumi kwenye vijiwe vya kahawa na kwenye vikao vya kinywaji kuhusu chanzo cha milipuko hiyo. Wakati mwingine watu wanageuza dhana zao kuwa ndiyo ukweli na kupotosha au hata kuwatia watu hofu. Wataalamu wamekwishafika, ukweli wenyewe utajulikana baada ya muda si mrefu.
Hali ya Chakula Nchini
Ndugu wananchi;
Jambo la pili ninalotaka kulisemea ni hali ya chakula nchini. Kwa ujumla hali ya upatikanaji wa chakula nchini katika maeneo mengi ni ya kuridhisha isipokuwa katika maeneo machache. Taarifa ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika inaonyesha kwamba kuna akiba ya kutosha ya chakula katika maghala ya Serikali, ya wafanyabiashara wakubwa na katika maghala ya wakulima mashambani. Maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula yana tani 216,012 za mahindi na mpunga, nafaka ambazo zinatuhakikishia kuwa upungufu wowote wa chakula tutaukabili bila matatizo. Kiasi hicho ndicho kikubwa kuliko chote kilichowahi kuhifadhiwa tangu hifadhi hiyo kuanzishwa na shabaha yetu ni kufikia tani 400,000 ifikapo mwaka 2015.
Ndugu wananchi;
Katika baadhi ya maeneo nchini kumeanza kujitokeza matatizo ya upungufu wa chakula kuanzia mwezi Januari 2011. Mengi ya maeneo hayo ni yale yanayopata mvua za vuli ambazo bahati mbaya hazikuwa nzuri. Imetambuliwa kuwa katika Halmashauri 36 za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara na Iringa ndiko kwenye maeneo mengi yenye upungufu mkubwa.
Tayari Serikali imeidhinisha kutolewa kwa jumla ya tani 13,760 za chakula kutoka Akiba ya Taifa ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kuhudumia watu 423,530 walioathiriwa na upungufu wa chakula katika maeneo hayo. Kazi ya usambazaji inaendelea. Hadi sasa jumla ya tani 4,822 za chakula cha msaada kimekwishatolewa katika mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro na Lindi. Napenda kuwathibitishia kuwa tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa. Tutawahudumia ipasavyo hawa waliokwishatambulika na wengineo watakaojitokeza siku za usoni.
Ndugu Wananchi;
Kwa sababu ya kukosekana kwa mvua za vuli na mvua kuwa pungufu katika maeneo mengine, mwelekeo wa hali ya upatikanaji wa chakula siyo mzuri sana. Tayari kiasi cha chakula kinachoingia kwenye masoko ya mijini si kingi kama ilivyokuwa siku za nyuma. Hii imekuwa kiini cha bei za vyakula kupanda katika masoko ya mijini. Hivi sasa matumaini yetu yapo kwa Mwenyezi Mungu kujaalia mvua za masika ziwe nzuri. Kama hilo halitatokea nchi yetu itakumbwa na tatizo kubwa la upungufu wa chakula na bei za vyakula kuwa kubwa zaidi. Tutajipanga ipasavyo kukabiliana na hali hiyo ili kunusuru maisha ya Watanzania. Ili kupunguza makali ya bei ya vyakula nimeagiza akiba ya taifa itumike kwa kuwauzia wafanyabiashara ya chakula mijini.
Ongezeko la Bei ya Sukari
Ndugu Wananchi;
Jambo la tatu ni bei ya Sukari. Hivi karibuni bei ya sukari nchini imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa na katika baadhi ya maeneo nchini bei ya sukari ilifika zaidi ya shilingi 2,200 kwa kilo. Nilimuomba Waziri Mkuu kufuatilia kwa karibu tatizo hilo na amefanya hivyo. Alikutana na wadau wote wakiwemo wazalishaji na wasambazaji wa sukari nchini. Kilichobainika ni kuwa bei ya sukari ilipanda sana kwa sababu ya kuwepo upungufu wa sukari katika soko. Upungufu wa sukari katika soko ulikuwa umesababishwa na sukari iliyokuwepo katika maghala ya viwanda vya sukari na ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari kutofikishwa kwa wingi madukani kwa hofu ambazo hazikuwa na msingi. Aidha, mahusiano mabaya kati ya wazalishaji na wafanyabiashara wakubwa wa sukari ilikuwa sababu kubwa. Wenye viwanda wakawa wanatoa kiasi kidogo kuliko wafanyabiashara walichokuwa wanaagiza. Kwa upande wao wafanyabiashara wakubwa nao wakawa wanasambaza kiasi kidogo kidogo kwa madai kuwa wasijekuishiwa kabisa na bidhaa hiyo.
Katika mazungumzo hayo ilibainika kuwa viwanda na wafanyabiashara wakubwa wanayo sukari ya kutosheleza mahitaji mpaka mwezi Mei, 2011. Kutakuwa na uhaba katika miezi ya Mei na Juni kutokana na ukweli kwamba viwanda vya sukari nchini husimamisha uzalishaji kuanzia mwezi Februari hadi Mei kila mwaka. Hiki ni kipindi cha mvua nyingi, miwa hunyonya maji mengi hivyo huwa haitoi sukari nyingi. Wenye viwanda hutumia muda huo kusimamisha uzalishaji na kufanya matengenezo ya mitambo.
Ndugu Wananchi;
Waziri Mkuu aliagiza sukari yote iliyoko katika maghala itoke mara moja na kufikishwa katika soko ili watu waipate tena kwa bei nafuu. Katika mazungumzo ya pamoja na wadau, ilikubalika kabisa kuwa hata kwa maeneo yaliyo mbali na viwanda vya sukari bei haiwezi kuzidi shilingi 1,700/= kwa kilo. Atakayeuza kwa bei kubwa zaidi ya hiyo anadhulumu, taarifa zitolewe ili hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kufutiwa leseni ya biashara.
Ndugu Wananchi;
Kwa ajili ya kuziba pengo la miezi ya Mei na Juni kibali kimetolewa cha kuagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi. Tunatarajia kupata tani 12,500 kutoka nchi za Afrika Mashariki na tani 37,500 zitatoka nje ya Afrika ya Mashariki. Bahati mbaya sana kuna upungufu mkubwa sana wa sukari duniani, hivyo bei imepanda kuliko wakati wowote katika miaka ya hivi karibuni. Tani moja ya sukari inauzwa kwa dola za Marekani 900 ikilinganshwa na dola za Marekani 500 mwaka 2009. Hivyo, sukari itakayoingizwa wakati huo itakuwa na bei kubwa. Kwa nia ya kuzifanya bei ziwe chini na kuwapa watumiaji nafuu, sukari hiyo haitatozwa ushuru wa forodha. Tutafanya hivyo pia kwa vyakula vyote muhimu tutakavyolazimika kuagiza kutoka nje kwa sababu ya uhaba wa mvua uliokumba maeneo mengi hapa nchini.
Hali ya Umeme
Ndugu wananchi,
Jambo la nne ni hali ya umeme. Kama mnavyofahamu, hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni mbaya. Chanzo cha matatizo ni kupungua sana kwa maji katika Bwawa kubwa la Mtera. Hadi jana kina cha Bwawa hilo kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7. Kwa sasa zimebaki mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.
Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. Baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi. Aidha, imesisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba wataoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa. Vile vile, watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.
Natambua kuwa Bodi na Mejemienti ya Shirika la Umeme, wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011.
Ndugu Wananchi;
Tulipopata tatizo kama hili mwaka 2006/2007 tuliamua kuwa tuanze safari ya kupunguza kutegemea mno umeme wa nguvu ya maji kwa kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati. Mpango umetengenezwa na utekelezaji wake unaendelea. Tayari umeme wa MW 145 wa kutokana na gesi asilia umeongezwa kwa kugharamiwa na Serikali. Aidha, mwisho wa mwaka huu MW 160 zitaongezeka yaani MW 100 Dar es Salaam na MW 60 Mwanza kwa gharama za Serikali.
Bahati mbaya kutokana na matatizo ya fedha ya kimataifa, wawekezaji wa sekta binafsi wa kuzalisha MW 300 za umeme wa gesi asilia pale Mtwara walijiondoa. Umeme huo ungekuwa tayari umeshaingizwa katika gridi ya taifa hivi sasa na kuondoa tatizo la sasa. Wawekezaji wengine wamepatikana na mazungumzo yanaendelea vizuri. Mradi wa Kiwira umecheleweshwa na mchakato wa kubadili milki na kupata mkopo wa dola za Marekani 400 milioni za kuwezesha ujenzi wa kituo cha kuzalisha MW 200. Suala la kubadili milki limefikia ukingoni na mchakato wa kupata mkopo unaendelea kwa matumaini.
Ndugu Wananchi;
Waswahili wana msemo usemao “jitihada za mwanadamu hazishindi kudra ya Mwenyezi Mungu”. Bahati mbaya sana tatizo la ukame limetukuta tena wakati mipango hiyo haijakamilika. Miaka miwili ijayo hali itakuwa tofauti sana kwani miradi hii na mingine kadhaa itakuwa imekamilika na kulihakikishia taifa uhakika wa umeme.
Naomba ndugu zangu muelewe kuwa miradi hii huchukua muda kukamilika. Mitambo huchukua muda kutengenezwa na ujenzi wa kituo nao pia. Ingekuwa ni mitambo ya kununua tu dukani tungefanya hivyo na kulimaliza mara moja tatizo hili. Tena lingeisha zamani na wala sisi tusingelikuta. Subira yavuta heri.
Hali ya Usalama Nchini
Ndugu Wananchi;
Hivi karibuni wananchi wengi wameingiwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa nchi yetu. Ni mara ya kwanza Watanzania wamekuwa hivyo. Hofu hiyo inatokana na kauli na vitendo vya wenzetu wa CHADEMA vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini. Kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia. Lakini, kuigeuza fursa hiyo kuwa ni jukwaa la kuchochea ghasia na kwa nia ya kuiondoa Serikali iliyoko madarakani kwa mabavu ni matumizi mabaya ya fursa hiyo.
Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila miaka mitano tunafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wetu. Uchaguzi wa mwisho tumefanya tarehe 31 Oktoba, 2010. Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. Kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na haya wanayoyazungumza sasa. Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama cha Mapinduzi. Iweje leo, miezi mitatu baadae kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni. Siyo sawa hata kidogo. Kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi.
Ndugu Wananchi;
Katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, mnapomaliza uchaguzi mmoja, mnajiandaa kwa uchaguzi mwingine. Mnajenga upya chama chenu, mnaongeza wanachama, mnaboresha sera na hoja zenu pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali nyinyi na kuwakataa wenzenu. Na, uwanja muhimu wa kufanya sehemu kubwa ya hayo ni katika Bunge na Halmashauri za wilaya kupitia Wabunge na Madiwani wenu.
Kuacha kufanya hivyo na badala yake kuamua kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ili muingie nyie ni kinyume kabisa na misingi ya demokrasia. Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima. Hebu fikirieni, kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani? Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida. Hatuitendei haki nchi yetu na hatuwatendei hai wananchi tunaodai tunawapenda na kuwatetea.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Ndugu zetu wa CHADEMA wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo. Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka. Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri. Wanataka kutumia mabavu. Naomba tuyakatae mambo yao. Tusiwafuate. Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. Sisi katika Serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea nayo kufanya kila siku. Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali. Kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, kikwazo kikubwa ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wetu na hivyo uwezo wetu siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo tunapenda iwe.
Ndugu Zangu;
Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo. Hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa. Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.
Lakini, pia ni muhimu watu kutambua ukweli kwamba uchumi kama wetu ambao haujajenga uwezo wake wa ndani wa kujitosheleza kwa mahitaji yake, huathirika sana nay ale yanayotokea katika uchumi wa dunia. Unapoyumba na sisi tunayumba. Bei za mafuta katika soko la dunia zikipanda na kwetu kupitia gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda. Mfumuko wa bei ukipanda China, nguo na bidhaa tunazonunua kutoka China hupanda bei. Hivi sasa mataifa yote makubwa tunakonunua bidhaa mfumuko wa bei umepanda na sisi tunaathirika. Mvua ikikosekana kunakuwa na uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula. Lawama kwa Serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi? Hata kwa matatizo yote hayo na mengine tumekuwa tunatafuta nafuu kwa kiwango tunachoweza. Aghalabu, hutoa nafuu ya kodi kama tulivyofanya kwa sukari na tulivyowahi kufanya kwa saruji na kadhalika. Tutaendelea kufanya hivyo inapobidi.
Mwisho
Ndugu Wananchi,
Naomba nimalizie kwa kuwashukuru wananchi kwa kuwa wavumilivu kwa kipindi chote hiki, nawaomba muendelee kuiunga mkono Serikali yenu. Tuendelee kuchapa kazi kwa bidii kuijenga na kuiendeleza nchi yetu na vile vile tuendelee kuithamini na kuitunza amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni sana kwa kunisikiliza!

Saturday, February 26, 2011
Rais wa TUSO IUCo ajiuzulu
Ni baada ya serikali yake kutuhumiwa ufisadi
![]() |
Rais John K. Juma akitoa ufafanuzi katika mkutano aliouitisha |
![]() |
Godwin Kunambi ambaye ni Katibu Mkuu wa Serikali ya wanafunzi aliyefukuzwa kazi akipanda jukwaani kutoa ufafanuzi |
![]() |
Kunambi akitoa vielelezo vya tuhuma za ufisadi wa serikali ya wanafunzi |
![]() |
Kwa msisitizo zaidi |
![]() |
Rais John K Juma akijiandaa kutoa utetezi wake |
![]() |
Wanafunzi walipovamia ofisi ya rais |
![]() |
Kunambi akijibu hoja za rais |
![]() |
Mashuhuda wa tukio |
![]() |
Kwa shauku kubwa |
![]() |
John K. Juma akitoa tamko la kijiuzulu |
![]() |
Mwandishi wa habari wa TBC, Lukra Zeno akichukua tukio |
Kunambi akizungumza na wanahabari |
Wakimtaka John K Juma atoke nje |
Wakisubiri hatima ya John Kanyoro Juu ya utawala wake |
Subscribe to:
Posts (Atom)